"Nimerejea katika ubora wangu," Messi awaambia mahasidi wake

messi-compressed
messi-compressed
Nahodha wa timu ya Barcelona Lionel Messi amesema kwamba amerejea kwa kishindo akiwa na matumaini zaidi kunyakua taji la ligi ya UEFA.

Akizungumza baada ya kuwasambaratisha Inter Millan kwa mabao  2-1, bingwa huyu wa dunia alionekana kumzungumzia nyota Mfaransa Antoine Griezmann ambaye uhusiano wao umekuwa baridi sana kutokana na sababu ambazo Messi hajaziweka bayana.

"Sina tatizo na Griezmann. Muda kwa muda uhusiano wetu unazidi kumarika," Messi alisema.

Messi ambaye hajakuwa na muda mzuri wa kucheza kutokana na jeraha la mguu alicheza kwa kipindi chote cha dakika 90 Jumatano.

"Nimefurahia kuwa na uwezo wa kucheza dakika zote 90 za kwanza msimu huu. Nilihisi kuchoka, lakini nilijizatiti kwa kuwa nilitaka kumaliza mchezo huu. Kwangu mimi ni muhimu sana kucheza michezo yote. Hivyo ndivyo ninavyojiandaa kwa michezo ijayo, kwa sababu ninayo michezo mingi iliyoratibwa na hatuna muda mwingi wa kufanya mazoezi." Messi alisema.

Kurejea kwa Messi katika mechi baada ya majereha kutaipa Barcelona nguvu na motisha unahitajika sana.

Nahodha huyu alizalishabao moja kati ya mabao 2 yaliyofungwa na nyota kutoka Uruguay Suarez katika dakika 58 na 84.