Hii ni kufuatia maneno ya utani yaliyotolewa na mlinzi huyo jumatatu jioni kuhusu mshambulizi huyo wa Juventus, katika sherehe za kumtuza mwanasoka bora duniani, al maarufu Ballon d’Or.
Van Dijk alimaliza wa pili, nyuma yake Lionel Messi ambaye alipokea tuzo hilo kwa mara ya sita sasa huku Ronaldo ambaye ameshinda tuzo hiyo mara tano akimaliza wa tatu.
Hata hivyo kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid hakuhudhuria sherehe hizo na badala yake alikuwa mjini Milan, Italia katika sherehe za 2019 Gran Gala del Calcio ambapo alituzwa kama mchezaji bora zaidi msimu uliopita katika ligi kuu ya Italia.
Mwanahabari mmoja alimuuliza Van Dijk iwapo kukosekana kwa Ronaldo kunamaanisha kuwa upinzani wa tuzo la Ballon d’Or umesalia kati yake na Messi pekee.
Kwa utani, Van Dijk aliuliza, 'Je, alikuwa mpinzani wakati huo?'