Wezi stadi wamefanikiwa kutoroka na mamilioni ya fedha kwa kudukua mashine za ATM. Udukuzi huu unajumuisha kueneza programu kwenye mitambo ya pesa na kusababisha kutoa kiasi kikubwa cha hela kwa mkupuo moja.
Akizungumza katika kongamano la uslama wa kimitandao na matumizi ya intaneti, Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i alisema kwamba kumekuwa na ongezeko la visa vya uhalifu mitandaoni, visa vya ulaghai kutoka watu bandia mtandaoni, usambasaji wa programu hasidi kwenye intaneti, udukuzi, na wizi wa kimitandaoni.
Visa hivi vimeweka Kenya katika ngazi ya juu kutokana na utovu wa usalama wa mitandaoni.
Kampuni inayotoa huduma za kudhibiti programu hasidi Kaspersky Security Network (IT Threat Evolution Quarter Two 2019) imeorodhesha taifa la Kenya kuwa miongoni mwa mataifa 10 yanayokabiliwa na athari hiyo.
Iran inaongoza kwa asilimia 28.31, ikifuatwa na Bangladesh kwa silimia 28.1 huku Kenya ikiwa nambari 10 kwa asilimia 15.38.
Hii hapa ni orodha ya nchi zilizoripotiwa kuwa na utovu wa usalama kwenye mitandao.
Asilimia
Nchi | % | |
1 | Iran | 28.31 |
2 | Bangladesh | 28.10 |
3 | Algeria | 24.77 |
4 | Pakistan | 24.00 |
5 | Tanzania | 23.07 |
6 | Nigeria | 22.69 |
7 | India | 21.65 |
8 | Indonesia | 18.13 |
9 | Sri Lanka | 15.96 |
10 | Kenya | 15.38 |
Zaidi ya visa milioni 26.6 viliripotiwa kati ya Aprili na Juni mwaka huu kulingana na Kituo cha Kitaifa cha kudhibiti visa vya mitandaoni.