Mechi hiyo almaarufu "Elclasico" imengojewa kwa hamu na mashabiki wa soka na leo hii baada ya dakika 90 itakuwa wazi bayana klabu gani bora zaidi.
Mara ya mwisho klabu hizo kuchuana Ernesto Valverde ambaye ni mkufunzi wa Barca alishinda mechi hiyo.
Barca itakuwa inategemea huduma za washambulizi Messi, Suarez, na Griezmann huku Real wakitegemea huduma za Benzema, Vinicious Junior na Toni Kroos.
Nani ataibuka mshindi? Yote hayo, yatathibitishwa leo.