Kimanzi asifu Eritrea baada ya Harambee Stars kunyukwa 1-4

eritrea
eritrea
Kocha wa Harambee stars Francis Kimanzi anasema kikosi cha Eritrea kilionyesha mchezo bora zaidi kuliko vijana wake jana baada ya kuwabwaga mabao manne kwa moja katika robo fainali ya kombe la CECAFA inayoendelea mjini Kamapala Uganda.

Stars walikua mabingwa watetezi walijipata taabani licha ya kushinda mechi zao zote za kwanza kwani vijana wa Red sea waliwaonyesha kivumbi.  Eritrea itacheza na Uganda katika fainali, baada ya wenyeji kuilaza Tanzania 1-0.

Kikosi ya Kenya cha riadha kwa vijana wasio zaidi umri wa miaka 20 kitakita kambi huko Nyeri kwa mazoezi ya mbio za dunia za mwaka 2020 kwa wanariadha wasiozidi umri wa miaka 20 zitakazoandaliwa Nairobi.

Wanariadha 50 wataelekea Nyeri, ili kuhakikisha kikosi hicho kiko imara zaidi.  Kenya itakua inawania kunyakua taji hilo.

Aston Villa ililaza Liverpool mabao 5-0 na kufuzu kwa nusu fainali ya kombe la ligi ya Uingereza, usiku wa jana ugani Villa Park. Huku kikosi cha kwanza cha  Liverpool kikiwa nchini Qatar  ambako watacheza na Monterrey katika kombe la klabu bingwa duniani, Liverpool walichezesha kikosi changa zaidi katika historia yao huku vijana wasio zaidi umri wa miaka 23 wakipiga shughuli.

Viongozi wa iigi ya Itaila  wameomba radhi kwa kutumia picha za nyani katika kampeini za kupambana na  ubaguzi wa rangi dhidi ya wachezaji weusi. Picha hiyo iliyonuia kuwaweka pamoja wachezaji imezua ghasia baada ya timu kadha zikiwemo AC Milan na Roma kudai kuwa hawaku husishwa katika kampeni hiyo na haikua bora.

Mchoraji aliyechora picha hiyo alidai alinuia kuwaweka wachezaji wa rangi zote sawa kwa kuwachora nyani hao mmoja mzuungu, mwengine wa kiafrika na yule wa ki Asia.

Kocha wa zamani wa Real Madrid, AC Milan  na Chelsea Carlo Ancelotti anatarajiwa kutajwa kama kocha mkuu wa Everton siku ya Alhamisi ama Ijumaa, baada ya kuafikiana na wenyeji kuchukua hatamu.

Mazungumzo yanaendelea baada ya mzaliwa huyo wa Italia kuwasili Uingereza, siku kadha baada ya kufutwa kazi kama kocha wa Napoli. Ancelotti atachukua  mahala pa Marco Silva ambaye alichujwa wiki mbili zilizopita.