logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pesa makaratasi! Ayub Timbe aonesha gari lake lenye dhamani ya 26M

Pesa makaratasi! Ayub Timbe aonesha gari lake lenye dhamani ya 26M

image
na

Burudani02 October 2020 - 10:03
Kiungo wa Harambee Stars, Atub Masika Timbe amewaacha marafiki na mashabiki wake wakiduwaa baada ya kulionesha gari lake la kifahari, gari ambalo wengi wetu huliona kwenye sinema tu.

Katika mtandao wake wa Instagram, Timbe anaoneka akiwa amekalia gari hilo la rangi ya kijani kibichi, lijulikanalo kama Lamborghini Huracan na linaaminika kumgharimu kitita cha zaidi ya shilingi milioni 26!

Timbe ambaye husakata kadanda katika klabu ya Beijing Renhe katika ligi kuu ya Uchina, alisherehekea siku ya kuzaliwa Jumanne iliyopita na tunakisia kuwa gari hilo la kifahari na lijulikanalo kwa mwendo wake wa kasi zaidi, lilikuwa kama njia yake ya kujizawadi.

Ujumbe wake ulikuwa,

If you Cant Stop thinking of it, Dont Stop working for it.✅✅

https://www.instagram.com/p/B2P1WNPpbRY/

Timbe ambaye sasa hivi yuko Uholanzi, alikuwa kwenye kikosi cha Kenya ambacho kiliiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la bara Afrika mapema mwaka huu, Misri.

Hayo yakijiri, Michael Olunga ambaye ni mshambulizi wa Harambee Stars amechaguliwa kama mchezaji bora wa mwezi uliopita wa Agosti wa timu yake, Kashiwa Reysol.

Kupitia Twitter, Olunga alimshukuru Mola, wachezaji wenzake na pia, mashabiki wake kwa kumuamini.

Aliandika,

I am happy to be elected August player of the month. I would like to thank God Almighty for His blessings. Without you it wouldn't be possible. My teammates, my supporters and everyone who believes in me,I am truly thankful All I can do is to continue working harder.

Hongera bwana Olunga!


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved