'Mashabiki wa Arsenal ndio walioniondoa,' Asema Unai Emery

Aliyekuwa meneja wa Arsenal Unai Emery anasema mashabiki wa Gunners "walimuondoa"katika klabu hiyo. (Marca - Spanish)

Msururu wa habari za michezo,

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy alisafiri hadi Uhispania kufanya mazungumzo na rais wa Real Madrid, Florentino Perez kufukuzia usajili wa winga wa Wales Gareth Bale, 30. (Times)

Leicester City wameonesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Southampton raia Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 24, ambaye kandarasi yake itakamilika katika kipindi cha miezi 18. (Ekstra Bladet - via Leicester Mercury)

Mshambuliaji wa Southampton Danny Ings, 27, alikuwa mada kuu kama mchezaji anayelengwa na Manchester United mwezi Januari. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Manchester United raia wa Serbia Nemanja Matic, 31, amekataa maombi ya kuondoka United na yuko tayari kuongeza kandarasi yake iwapo klabu hiyo itaamua kufanya mazungumzo naye. (Telegraph)

Mlinzi wa England Ashley Young, 34, aliyejiunga na Inter Milan kjwa mkopo kutoka Manchester United mwezi January, amesema Antonio Conte alijaribu kumsajili alipokuwa meneja wa Chelsea. (Sky Sports)

Carlo Ancelotti amesema Everton itakuwa na wakati rahisi kukataa maombi ya Richarlison iwapo kutatumwa maombi ya kuhamia klabu nyengine wakati ujao. Raia huyo wa Brazil, 22, alikuwa anahusishwa na kuhamia Barcelona wakati wa dirisha la usajili. ( Liverpool Echo)

-BBC