Michezo,Kyle Walker mashakani baada ya kukiuka amri ya serikali

68962250_741265749637113_349360974928788160_n
68962250_741265749637113_349360974928788160_n
NA NICKSON TOSI

Mlinzi wa  klabu ya Manchester City  Kyle Walker yupo matatani ya kuadhibiwa na klabu hiyo ya Uingereza baada ya kukiuka amri ya serikali ya kupiga marufuku ya watu kutotoka nje wakati huu ambapo Uingereza inakabiliana na Corona .

Walker anadaiwa  kuandaa sherehe katika boma lake na marafiki wake wa karibu wakiwemo warembo wawili katika nyumba yake iliyoko Cheshire siku chache tu baada ya kuwarai wananchi wa taifa hilo kuheshimu amri ya Serikali.

Walker baada ya kukiri makosa hayo aliomba radhi kupitia taarifa aliyoichapisha kwenye gazeti moja la humo nchini na kusema kuwa aliiandaa sherehe hiyo akiwa na marafiki wake kutoka kwa familia ,wa klabu na hata wale wanaoshabikia mchezo wake .