Tutafanya Usajili wa kutosha msimu huu ukimalizika –Ole Gunnar Solkjaer asema.

NA NICKSON TOSI

Meneja mkuu wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar amesema kuwa, licha ya ligi kuu ya Uingereza kusitishwa kutokana na janga la Corona, klabu yake ya Manchester imejiandaa vyema ili kusajili wachezaji ambao wamekuwa wakiwaangazia msimu huu wote.

Akizungumza na shirika la michezo la Sky Sport, Ole amesema kuwa mikakati yote imewekwa ili kuhakikisha kuwa klabu hiyo inasajili wachezaji ambao wataifanya United kukabiliana na ushindani kutoka kwa vilabu vingine mahasidi.

Wakati uo huo, Solkjaer amesema hatua ya kusitishwa kwa ligi kuu ya Uingereza kumefanya wachezaji kama Marcus Rashford na Paul Pogba kupata nafuu baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na majeraha ambayo walipata mwanzoni mwa msimu. Ameongeza kuwa, kurejea kwa wachezaji hao kutapiga cheki kikosi chake iwapo ligi itarejelea hali yake ya kawaida.

United wamekuwa wakihusishwa na usajili wa wachezaji Jack Grealish na Jordan Sancho