Michezo! Wachezaji wa Arsenal wakataa kupunguza mishahara yao

NA NICKSON TOSI

Kikosi cha Kwanza cha Arsenal kimepusilia mbali pendekezo la Usimamizi wa klabu hiyo la kutaka kupunguziwa mshahara wao kwa asilimia 12.5 kwa muda wa mwaka mmoja kufuatia hasara waliyosajili wakati huu ambapo hakuna shughuli zozote za  ligi kuu ya Uingereza zinazoendelea.

Hatua ya kupunguza mshara wa wachezaji wa Arsenal ilionekana kama ya kupunguzia gharama uongozi wa klabu hiyo haswa wakati huu ambapo ligi takriban zote ulimwenguni zimesitishwa kutokana athari ambazo zimetokana na Corona.

 Baadhi hya wachezaji wanaolipwa mishahara nono katika klabu hiyo ya Ungereza ni Mesut Ozil anayelipwa £350,000, Pierre-Emerick Aubameyang na  Alexandre Lacazette  £200,000 .

Ligi kuu ya Uingereza ilisitishwa baada ya wachezaji na mameneja wa timu mbalimbali kupatikana na virusi vya Corona, hali iliyofanya shirikisho la soka la Uingereza FA na usimamizi wa Premier league kusitisha ligi hiyo kwa ghafla.

Aidha timu na wachezaji wamekuwa wakishauriwa na wakuu wa serikali kukubali kupunguziwa mishahara kwa asilimia 30 ili kutoa mchango kwa serikali kufanikisha shughuli za kutoa huduma kwa wananchi wa taifa hilo ambalo limeathirika pakubwa na virusi vya Corona.