Hueng Min Son aanza majukumu rasmi ya kijeshi Korea Kusini

NA NICKSON TOSI

Mshambulizi wa Tottenham Heung-Min Son ameanza rasmi majukumu yake ya kutumikia taifa kama mwanajeshi baada ya kumaliza siku 21 akiwa kwenye karantini.

Hueng Min Son kuendelea na shughuli za kijeshi – Serikali ya Korea Kusini yasema

Mchezaji huyo wa miaka 27 anafanya kazi na kitengo cha Marine corps katika kisiwa cha Jeju ambapo ataendelea na mazoezi yake.

Katika mojawapo ya masharti ya taifa la Korea Kusini ni kuwa iwapo wewe ni mwanamume ambaye huna matatizo yoyote utahitajika kufanya kazi aghalabu kwa mwaka mmoja katika vikosi vya majeshi ya nchi hiyo.

Atakapokuwa akisherekea miaka 28, mchezaji huyo atakuwa akiendelea na mazoezi na wenzake katika kisiwa cha jeju.