Jaro Soja aanza kuwatengenezea mashabiki wa Gor Mahia maski

IMG_20200421_130629-scaled
IMG_20200421_130629-scaled
NA NICKSON TOSI

Kutokana na kusitishwa kwa ligi ya humu nchini na nyingine nyingi duniani kutokana na Corona, Jaro Soja shabiki anayefahamika sana kutokana na mbwembwe zake wakati klabu ya Gor Mahia inapocheza, amesema kuwa hatua hiyo imemfanya kuanza mradi wa kutengeneza maski na kuwapatia mashabiki wa Gor ambao hawana uwezo wa kununua barakoa hizo.

Ubunifu wake wa kutengeneza barakoa unajiri siku chache tu baada ya waziri wa afya Mutahi Kagwe kutoa amri kila mkenya kuvalia vizuizi hivyo na kusema kuwa atakayepatikana akiwa hana maski atachukuliwa hatua na kulazimika kutoa faini ya shilingi 20,000 ama kufungwa gerezani.