Romelu Lukaku aomba msamaha Klabu ya Intermilan kutokana na usemi wake

skysports-romelu-lukaku-inter-milan_4900963
skysports-romelu-lukaku-inter-milan_4900963
NA NICKSON TOSI

Mshambulizi wa klabu ya Intermilan Romelu Lukaku ameomba radhi kutokana na matamshi yake kuwa wachezaji wa timu hiyo 23 kati ya 25 walikuwa miongoni mwa waathirika wa gonjwa la Corona ambalo linaendelea kutikisa taifa la Italia.

Hakuna mkuu wa Klabu hiyo aliyokuwa amethibitisha taarifa hiyo japo Lukaku akiwa kwa mahojiano na televisheni ya Ubelgiji alisema baada ya wachezaji kurejea kutoka kwa likizo ya muda mfupi, baadhi yao walikuwa wanaonyesha dalili za virusi hivyo.

Lukaku baada ya kuomba msamaha huo, uongozi wa timu hiyo umeamua kumuadhibu kutokana na maoni hayo na kusema kuwa wameshangazwa na hatua ya mchezaji huyo.

Taifa la Italia ni miongoni mwa mataifa ambayo yameathirika zaidio kutokana na virusi vya corona huku maelfu ya watu wakiwa wamepoteza maisha yao.

Kisa cha kwanza kiliripotiwa kwenye taifa mnamo Januari 31.