Liverpool yasingizia klabu ya Athletico Madrid kuwa ilichangia pakubwa kuenea kwa Corona katika mjini humo

NA NICKSON TOSI

Katika tukio la kustaajabisha malimwengu ya Soka ni kuwa mkuu wa mji wa Liverpool Steve Rotheram sasa amewataka wasimamizi wa dimba la ligi ya mabingwa kuanzisha uchunguzi kubaini iwapo Athletico Madrid ilichangia pakubwa kusambaa kwa virusi vya Corona ambavyo vimeathiri mji huo.

Mtanange wa makundi awamu ya 16 bora uliochezwa Machi 11 na ambao klabu hiyo ililazwa magoli 3-2 na kutolewa na kubanduliwa nje ya dimba hilo na kushuhudiwa na mashabiki takriban 52, 000, wale waliotoka Uhispania wakiwa 3,000.

Baada ya mchuani huo, taifa la Uhispania lilifunga shughuli zote za spoti kutokana na mkurupuko wa virusi hivyo ambavyo vilikuwa vimeanza kuathiri maelfu ya watu.

Mshauri wa utafiti katika serikali kuu ya Uingereza Angela McLean amesema matamshi ya kiongozi huyo ni ya kustaajabisha sana na kueleza kuwa ameshangazwa na madai hayo.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO