Wachezaji wa ligi kuu Uingereza kuvalia maski wakiwa mazoezini

skysports-gremio-face-mask_4948379
skysports-gremio-face-mask_4948379
NA NICKSON TOSI

Wachezaji wanaoshiriki ligi kuu ya Uingereza watalazimika kuvalia maski wakiwa mazoezini kutokana na sheria mpya zilizoafikiwa na uonmgozi wa ligi hiyo wakati ambapo wanapania kurejelea mechi ambazo zilikuwa zimesalia,jarida la Daily Mail limeripoti.

Aidha sheria hiyo mpya itaangaziwa pakubwa katika mkutano wa vilabu hiyo kesho.

Mapendekezo hayo yamebuniwa na mkurugenzi wa michezo ligi kuu ya Uingereza Richard Garlick japo kurejea kwa mazoezi na wachezaji kutafanyika tu iwapo serikali itakubali.

Miongoni mwa masharti mengine yanayopendekezwa ni wachezaji kufanyiwa vipimo na maafisa wengine saa  48 kabla ya kurejelea mazeozi.