SHAMEFULL! Salomon Kalou apewa likizo ya lazima na klabu yake

Kalou-1-e1588619290205
Kalou-1-e1588619290205

NA NICKSON TOSI

Mchezaji wa klabu ya Hertha Berlin Salomon Kalou ametumwa kwa likizo ya lazima na klabu hiyo baada ya kuonekana kwa video akiwasalimu wachezaji wenza kinyume na masharti yaliyowekwa na serikali na hata usimamizi wa timu hiyo wakati huu ambapo mataifa mengi yanakabiliana na corona.

Kalou pia alionekana katika video hiyo akihitilafiana na shughuli ya kupima mchezaji mwenza Jordan Torunarigha huku akionekana akimlazimisha kumsalimu.

 Kalou mapema mwezi huu alikuwa amelalama kuhusiana na hatua ya klabu hiyo kuwapunguzia mishahara ya wachezaji swala ambalo limechangia pakubwa usimamizi wa klabu hiyo kumpatia likizo ya lazima.

“With this video taken inside the team’s dressing room, Kalou broke clear internal rules and displayed a behaviour, which is neither appropriate for this current situation, nor reflective of the code of conduct of Hertha BSC,“The club has therefore made the decision to suspend the player in question from training and matches with immediate effect.”taarifa iliyotumwa na uongozi wa HerthaBerlin.

Meneja Mcheal Preetz amesema Kalou hajaikosea tu klabu hiyo ya Hertha Berlin japo ametuma ujumbe kuwa wachezaji hawatilii maanani masharti yaliyowekwa na serikali na kuongeza kuwa huenda swala hilo likafanya ligi kusimamishwa.

Aidha Kalou kupitia kwa mtandao wake ameomba msamaha.