Kwenda Kabisa! Shimanyula amtaka Nick Mwenda kung'atuka afisini

NA NICKSON TOSI

Mwenyekiti wa klabu ya Kakamega Homeboyz Cleophas Shimanyula sasa ametaka kiongozi wa FKF Nick Mwendwa kung'atuka afisini baada ya kuwatangaza Gor Mahia kama washindi wa ligi kuu ya humu nchini msimu 2019/2020.

Mwendwa aliafikia uamuzi huo wiki jana na kuanzisha vita vingine dhidi yake na viongozi wa KPL.

Aidha, Shimanyula ambaye timu yake ilikuwa inshikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa KPL na alama 47 nyuma ya Gor Mahia ambao walikuwa na alama 54 anamtaka kiongozi huyo kuondoka afisini.

“Mwendwa’s time to leave office lapsed long time ago, he is the reason why football is ailing in Kenya. He has hurriedly ended this season’s league fearing for Kariobangi Sharks potential relegation,” amesema Shimanyula.

Kariobangi Sharks ambayo ni timu inayomilikiwa na Mwendwa inashikilia nafasi ya 12 .

Yakijiri hayo, mwenyekiti wa AFC Leopards Dan Shikanda sasa ametishia kuwa ataelekea katika mahakama za kutatua mzozo wa michezo nchini kupinga uamuzi huo wa Mwendwa.

Wenyekiti wa vilabu vingine pia wametofautiana  vikali na uamuzi wa Mwendwa, akiwemo Elly Kalekwa wa Sofapaka ambaye alishangazwa jinsi uamuzi huo ulivyoharikishwa kufanywa.

Mwendwa should have first of all consulted with the Kenyan Premier League before jumping to the a conclusion,” amesema Kalekwa .