Mnilipe ama msahau huduma zangu! Mapigano awaambia Gor Mahia

mapigano_pix
mapigano_pix

NA NICKSON TOSI

Mlinda lango wa Gor Mahia David Mapigano ambaye anatokea taifa jirani la Tanzania amewaambia mabingwa hao wa humu nchini kuwa hatarejea nchini hadi pale atakapolipwa senti zake.

Mapigano amewaambia viongozi wa timu hiyo kuwa hakuna mazungumzo yoyote yatakayofanyika kuhusiana na kuongeza mkataba wake kama bado hawajamlipa malindikizi ya mshahara wake wote.

Inadaiwa kuwa Gor haijawalipa wachezaji kwa muda wa miezi saba sasa na huenda asilimia kubwa ya wachezaji wakafunganya na kutafuta makao mengine.

Swala la wachezaji kukosa kulipwa katika klabu ya Gor imechangiwa pakubwa na kukosekana kwa mdhamini baada ya Sportpesa kufanganya.

Aidha Mapigano aliyesajiliwa na Gor kutoka klabu inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania ya Singida amekaidi kuwa hatarejea klabuni humo iwapo donge lake halitawekwa kwa akaunti yake.

Kulingana na mkataba uliotiwa saini baina yake na Gor ni kuwa utakamilika mwaka 2021 Julai.