Meya wa London apinga hatua ya ligi kuu ya Uingereza kurejelea mechi zake

Meya wa jiji kuu la Uingereza London, Sadiq Khgan amepinga vikali hatua ya wasimamizi wakuu wa ligi kuu ya Uingereza 'Premier League' kutaka mechi zilizokuwa zimesalia kurejelewa ifikiapo Juni Mosi akisema watu wengi katika taifa hilo wanaendelea kupoteza maisha yao huku wengine wakiendelea kuambukizwa.

Hiyo jana, washikadau wa michezo Uingereza kwa kauli moja walikubaliana kurejelewa kwa ligi hiyo kuanzia Juni 1 ili kumalizia msimu huu wa 2019-2020.

“Sadiq is extremely keen for the Premier League and professional sport in general to resume,” “However, with the country still in the grips of this crisis, and hundreds of people dying every day, he believes that it is too early to be discussing the resumption of the Premier League and top-flight sport in the capital.” amesema msemaji wa Meya Sadiq

Miongoni mwa vilabu ambayvo huenda vikanufaika na urejeo wa ligi hiyo ni Arsenal, Chelsea na Tottenham kwani wasimamizi wa ligi hiyo walikadiria kuwa viwanja kutoka London ndivyo vitakavyotumika ili kupunguza usafiri wa timu ambao unaweza kuchangia kusambaa kwa corona.

Uingereza ni miongoniu mwa mataifa yaliyoathirika pakubwa Ulaya huku ikiwa na visa 32, 000 vya watu kufa kutokana na corona na watu wengine 223, 000 wakiwa wameambukizwa.