Hamilton aongoza Uingereza kama mwanaspoti tajiri zaidi -Sunday Times

Bingwa mara sita wa mashindano ya Formula One Lewis Hamilton anaongoza kama mwanaspoti tajiri zaidi Uingereza chini ya miaka 30 na zaidi akiwa na kima cha bilioni 29, taarifa ambazo zimechapishwa na jarida la Sunday Times.

Hamilton ambaye alitia mkataba mwingine na kampuni ya Mercdes mwaka 2018 hupokea kima cha biloni 5.2 kila mwaka, mshahara ambao uliongezeka na blioni 4.8 mwaka jana.

Mchezaji wa kimataifa wa Wales na klabu ya Real Madrid Gareth Bale ambaye hulipwa milioni 46 kila wiki baada ya kutozwa ushuru anasemekana ana kima cha hela bilioni 14.8 akiwa mchezaji wa pekee kutoka UK mwenye umri wa miaka 30 na ama chini mkwasi zaidi.

Takwimu hizo ambazo zimetolewa na jarida la Sunday Times linaangazia mishahara ya wachezaji walioa na miaka 30 ama chini yake.

Mwanamaswimbi Anthony Joshua alijipatia bilioni 10 kutokana na pigano lake la hivi karibuni na Andy Ruiz Jr na kumfanya kuwa na bilioni 14.

Kulingana na Sunday Times, wafuatao ndio wanaspoti tajiri wa miaka ama chini ya miaka 30.

1. Gareth Bale (football) 14.8 billion

2. Anthony Joshua (boxing) 14 billion

3. Paul Pogba (football) 6.5 billion

4= Kevin de Bruyne (football) 4.4 billion

4= David de Gea (football) 4.4 billion

6. Raheem Sterling (football) 3.7 billion

7. N’Golo Kante (football) 3.3 billion

8. Harry Kane (football) 3.1 billion

9. Daniel Sturridge (football) 2.9 billion

10. Jordan Henderson (football) 2.7 billion