Tetesi za Uhamisho katika ligi za Ulaya - Michezo

_112303526_f8469875-4940-4db9-a488-f44dd6f10127
_112303526_f8469875-4940-4db9-a488-f44dd6f10127
Real Madrid bado wana nia ya kumnunua Erling Braut Haaland na watamfuatilia mshambuliaji huyo wa miaka 19- leo Jumamosi wakati Borussia Dortmund watarejea uwanjani katika ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga.

Manchester City wanajiandaa kumpatia mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus mkataba mpya wa thamani ya £120,000 kwa wiki kuzuia nyota huyo wa miaka 23 asinyakuliwe  na Juventus.

Lakini City wanataka kumuuza kiungo mshambulizi wa kati Leroy Sane msimu huu, licha ya masharti yao makali dhidi ya Bayern Munich kuhusu uhamisho wa Mjerumani huyo wa miaka 24. Mkataba wa Sane unaingia miezi 12 ya mwisho mwishoni mwa msimu

Kiungo wa kati wa Ujerumani Toni Kroos, 30, amepuuzilia mbali uwezekano wake kuungana tena na Pep Guardiola. Manchester City amesema kuwa anatarajia kukamilisha taaluma yake ya soka katika klabu ya Real Madrid.

Newcastle wanafanya mazungunzo kuhusu uhamisho wa thamani ya £21.25m ya nyota wa Inter Milan Valentino Lazaro baada ya winga huyo wa Austria kuonesha umahiri wake alipokuwa wakicheza kwa mkopo katika klabu hiyo msimu huu.

Mkufunzi wa zamani wa Gunners Unai Emery anadai kuwa alilazimishwa kumsajili winga Nicolas Pepe, 25, kujiunga na Arsenal na kufichua kuwa alimtaka mshambuliaji Wilfried Zaha, 27, baada ya kufanya mazungumzo na nyota huyo wa Crystal Palace.

Leicester City hawana mpango wa kumuuza Wilfred Ndidi katika dirisha la uhamisho la wachezaji litakapofunguliwa licha ya tetesi inayomhusisha kiungo huyo wa kati wa Nigeria wa miaka 23 na mamba wa Ufaransa Paris St-Germain na Manchester United.