Mabingwa hao wa Uingereza walipatikana na makosa ya udanganyifu kuhusiana na matumizi ya pesa na kupewa marufuku hayo na Uefa, makosa ambayo sasa City imesema ni uongo.
Mahakama hiyo sasa imesema baadhi ya vikao vitakuwa vikifanyika kupitia njia ya video kutokana na hofu ya virusi hatari vya corona.
“some hearings may be conducted by video conference” because of the travel restrictions in place because of the coronavirus pandemic.''
Uefa ilianzisha uchunguzi baada ya jarida moja la Ujerumani kufichua taarifa zinazoonyesha jinsi City walivyotumia pesa mwaka 2018 zikiwemo za ufadhili, ambapo zilitofautiana na zile walizowasilisha mbele ya tume ya kuratibu viwango vya matumizi ya pesa kwa vilabu.