PSG yatuma ombi rasmi la kumsajili mshambulizi Mauro Icardi

Mabingwa wa Ufaransa PSG wamewasilisha dau la milioni 44.5 ili kupata huduma za mshambulizi wa Argentina Mauro Icardi.

PSG imewasilishs dau hilo huku kukiwa na nyongeza ya milioni 8.9 katika klabu yake yae Intermilan.

Icardi amekuwa kwa mkopo katika mabingwa hao wa Ufaransa tangu msimu jana na palikuwepo na makubaliano pande zote mbili ya uwezekano wa kumnunua mshambulizi huyo.

Taarifa hizi zinajiri huku maisha ya Edinson Cavanni katika klabu hiyo ya PSG yakiwa haiyajabainika baada ya mkataba wake kukamilika.