Mikel Kiprotich Mutai apigwa marufuku ya miaka 4 kwa kutumia dawa za kutitimua misuli

Doping
Doping
Jaribio la Kenya kutaka kuzuiya matumizi ya dawa za kutitimua ama kusisimua misuli na wanariadha nchini limepata pigo baada ya shirika la Athletics Integrity Unit AIU kumpiga marufuku ya miaka 4 mwanariadha wa masafa marefu Mikel Kiprotich Mutai kwa matumizi ya dawa hizo.

Yakijiri hayo pia mwanariadha mwengine Japheth Kipchir chir Kipkorir amepigwa marufuku kwa kutumia dawa zilizokuwa zimekatazwa  na shirika hilo.

AIU ilitoa taarifa hiyo ya kumpiga marufuku Mutai kupitia ukurasa wao wa Twitter .Marufuku hayo sasa yataanza kutekelezwa  kuanzia mwezi huu.

Shirika la Anti Dopping Agency la kenya ADAK na lile la riadha nchini Athletics Kenya kwa miaka miwili sasa yamekuwa yakieneza hamasisho ya kuwataka wanariadha wa humu nchini kukoma kutumia dawa hizo.