Ufaransa yataka ufafanuzi zaidi wa kumalizika kwa ligi mapema

03fb6da73b317c42f84a390897f275d79b9ea214
03fb6da73b317c42f84a390897f275d79b9ea214
Mzozo umeanza kuibuka baina ya serikali na usimamizi wa ligi kuu ya Ufaransa French League 1 baada ya wakuu wa ligi hiyo kutangaza kumalizika kwa msimu 2019/2020 zikiwa zimesalia mechi 10 kutokana na virusi vya corona ambavyo vimeathiria taifa hilo.

Hatua ya serikali ya kutaka ufafanuzi zaidi kuhusiana na hatua hiyo inajiri baada ya ligi zingine ulimwenguni kama Bundesliga,Premier League na Serie A zikipania kurejea wiki lijalo .

Uamuzi wa kusitishwa ligi kuu ya Ufaransa umetajwa kama wa kiupuzi na serikali na sasa wanataka washikadau katika ligi hiyo kufafanua ni kwa nini uamuzi uliafikiwa mapema.

“Like idiots” was the headline on the front of L’Equipe on Friday, as the sports daily questioned why such a hasty decision was made by the league (LFP) to end the season.taarifa ya serikali.

Hata hivyo wasimamizi wa ligi hiyo wamesema kuwa waliafikia kuchukuwa hatua hiyo baada ya waziri mkuu kuongezea makataa ya watu kutotangamana eneo moja ili kuzuiya maambukizi Aprili mwaka huu.

Kufikia sasa Ufaransa imesajili vifo vilivyotokana na corona takriban 29000,idadi kubwa kuliko Ujerumani japo ndogo zaidi kuliko Uingereza,Amerika ,Uhispania na Brazil.