logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Michezo ya shule za upili kufanyika mwakani

Michezo ya shule za upili kufanyika mwakani

image
na

Burudani02 October 2020 - 07:52
Kakamega-High-Dagoretti-High-School-Rugby-15s
Michezo ya shule za upili ukanda wa Afrika Mashariki na iliyokuwa inaratibiwa kufanyika mwaka huu sasa itafanyika mwaka ujao 2021 kutokana na virusi vya corona vilivyositisha shughuli nyingi.

Mashindano hayo ya kila mwaka yalikuwa yameratibiwa kuanza kufanyika Agosti 14 hadi 24 katika kaunti ya Kakamega japo mkutano ulioandaliwa kati ya International Sports Federation ukiongozwa na rais wake Laurent Petrynka na katibu mkuu wa shirika la FEASSSA secretary David Ngugi uliamua kuafikia kufanyika kwa mashindano hayo mwaka ujao.

Ngugi ambaye pia ni katibu mkuu wa shirikisho la michezo ya shule za upili humu nchini Kenya Secondary School Sports Association (KSSSA), alisema kuwa itakuwa vigumu kufanyika kwa mashindano hayo mwaka huu kutokana na virusi hivyo.

“We’ve made a decision to postpone the championship until next year because of the health challenge the world is facing. Kenya remains the host of the postponed games and it will be bigger next year because the ISF president has promised us he will attend. Also, the president has said that ISF has rescheduled the World Games to next October, ” Ngugi .

Kwa upande wake mwenyekiti wa shirika la ISF  Petrynka amesema watashirikiana na mataifa husika katika mashindano hayo ili kuhakikisha kuwa wanapigana na virusi hivyo hatari.

 “I urge all countries to plan for the resumption of sports activities once schools are re-opened because all over the world, sports form an integral part of the learning process. We’re also keen on development of school sports in Africa, “Petrynka.

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved