Bayern washinda taji la 8 mfululizo

Ushindi telezi wa Bayern Munich wa 1-0 dhidi ya Werder Bremen Jumanne, Juni 16 usiku, umewapelekea kutwaa taji lao la nane Bundesliga.

Bao la dakika ya 43 la Robert Lewandowski ndilo lilileta tofauti na kumshuhudia Alphonso Davies akilishwa kadi nyekundu kipindi cha pili.

Wakiwa na tofauti ya pointi saba mbele ya mahasimu wao wa jadi Borussia Dortmund ikiwa imesalia mechi tatu, Bayern ilihitaji ushindi mmoja tu kutawazwa mabingwa.

Ushindi dhidi ya Bremen ilirefusha uongozi wao na pointi 76 ambayo ni mwanya mkubwa kwa Dortmund kuwafikia.

Klabu hiyo bado haijapoteza mechi yoyote tangu kurejea kwa Bundesliga, huku ikishinda mechi zote saba iliyoshirki.

Japo walisajili matokeo mabovu katika mechi yao ya Jumapili, bado wataridhika na matokeo yao ya mwisho.

Aidha, wanatakiwa kumpongeza mlinda lango wao Manuel Neuer baada ya kupangua mkwaju kwa ubunifu kabla ya mechi hiyo kutamatika na kukuza uongozi wao.

Wakati uo huo, taji hilo la nyumbani ni ishara kuwa Bavarians ni klabu cha pili katika orodha ya vilabu tano bora kushinda taji lao la nne kwa mpigo baada ya Juventus ambao walisajili historia hiyo 2011/12 hadi 2018/19.