Ibrahim Shikanda atimuliwa na Bandari fc

Klabu ya Bandari nchini imemfuta naibu mkufunzi wa timu hiyo Ibrahim Shikanda kama njia ya kupunguza gharama ya malipo kutokana na madhara yaliyosababishwa na virusi vya corona.

Shikanda amesema kuwa alipigiwa simu na kuarifiwa swala hilo na uongozi wa timu hiyo.

“It’s true I am no longer part of the Bandari technical bench, I was called by the club’s management and they informed me that owing to the effect of the Corona Virus they want to reduce the number of people on the technical bench.“I accepted the decision and I will be looking forward to make a quick comeback in football once these pandemic is under proper control,”Shikanda .

Shikanda na  Nassor Mwakoba walikuwa kama manaibu kocha chini ya uongozi wa mkufunzi Bernard Mwalala ambaye pia alionyeshwa mlango huku Twahir Mhidini akiteuliwa kuiongoza klabu hiyo mnamo Januari mwaka huu kabla ya Ken Odhiambo kuchukua hatamu hizo rasmi.

Mmoja wa bodi ya Bandari amesema kuwa wafadhili wao ambao ni halmashauri ya bandari nchini iliwataka kupunguza baadhi ya wafanyakazi wake kutoka 38 hadi 30.

“We were told to minimise our squad to accommodate only 30 from our current 38 people.”