Leo ni siku ya kiama katika ligi kuu ya Uingireza

Mbivu la mbichi itajulikana leo wakati ligi kuu ya primia nchini Uingereza inapofika tamati.

Baada ya kila timu kucheza jumla ya mechi 37 kila timu imesalia na mechi moja na kama ilivyo desturi mechi zote zitasakatwa kwa wakati mmoja.

Liverppol tayari ilitawazwa mshindi wa kombe hilo msimu huu huku Manchester City ikijihakikishia nafasi ya pili.

Kinyanganyiro hata hivyo ni kati ya nambari tatu Manchester United, Nambari nne Chelsea na Leicester iliyo katika nafasi ya tano zinapong'ang'ania nafasi za nne bora ili kujikatia tiketi za kushiriki ligi kuu ya mabingwa barani ulaya msimu ujao.

Manchester United inahitaji sare ya aina yoyote dhidi ya Leicester City wakati timu hizo zitakapokutana ili kujikatia tiketi katika dimba la ligi ya mabingwa msimu ujao. Mancheter United ina alama 63, alama sawa na Chelsea inayodunishwa kwa idadi ya mabao.

Leicester City inashikilia nafasi ya tano kwa alama 62 na ushindi dhidi ya Manchester United utaipa nafasi ya kushiriki dimba la ligi ya mabingwa.

Chelsea itakuwa na kibarua cha ziada dhidi ya Wolverhampton ikilenga kusajili alama tatu ili kujihakikishia nafasi katika kipute cha ligi ya mabingwa barani Uropa. Ikiwa Chelsea itatoka sare basi itahitaji kuiombea Manchester United ilaze Leicester City kwani sare ya aina yoyote itakuwa furaha kwa Leicester ikiwa itatoka sare na Manchester United.

Katika mechi zingine Arsenal itamenyana na Watford, Manchester City ipambane na Norwich ambao tayari wameteremshwa ngazi, Newcastle ialike mabingwa Liverpool huku Totenham ikiwa ugenini dhidi ya Crystal Palace.

Msimamo wa ligi kabla ya mechi za awamu ya 38

Team Pl W D L F A GD Pts
1 37 31 3 3 82 32 50 96
2 37 25 3 9 97 35 62 78
3 37 17 12 8 64 36 28 63
4 37 19 6 12 67 54 13 63
5 37 18 8 11 67 39 28 62
6 37 15 14 8 51 38 13 59
7 37 16 10 11 60 46 14 58
8 37 14 12 11 38 36 2 54
9 37 15 9 13 42 48 -6 54
10 37 13 14 10 53 46 7 53
11 37 13 10 14 43 53 -10 49
12 37 14 7 16 48 59 -11 49
13 37 11 11 15 37 55 -18 44
14 37 11 9 17 30 49 -19 42
15 37 10 8 19 48 61 -13 38
16 37 8 14 15 37 53 -16 38
17 37 9 7 21 40 66 -26 34
18 37 8 10 19 34 61 -27 34
19 37 8 7 22 37 64 -27 31
20 37 5 6 26 26 70 -44 21