logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Man United yaicharaza Leicester City na kufaulu miongoni wa timu,4,bora

Man United yaicharaza Leicester City na kufaulu miongoni wa timu,4,bora

image
na

Yanayojiri01 October 2020 - 11:02
Mechi kati ya Leicester City na Man United  iliochezwa mnamo tarehe 26,Julai, iliwashuhudia Mashetani Wekundu kuingia kwenye ligi ya mabingwa,Mabao mawili awamu ya pili kutoka kwa Lingard na Fernandes yalitosha kuzima Leicester.

Man United wameshikilia katika nafasi ya tatu na pointi,66,huku wakifuatwa na timu ya Chelsea katika mtanange wa uropa.Mechi hiyo ya mwisho ya msimu wa 2019/20 ilikuwa na kibarua huku upande zote zikipigania kumaliza kwenye nafasi ya nne bora.

Mashetani Wekundu walikuwa na imani kuwa droo itawatosha kuingia katika mashindano ya bara Uropa licha ya matokeo ya mechi kati ya Chelsea na Wolves. United walionekana kujivuta awamu ya kwanza katika uwanja wa King Power huku wenyeji wakitawala mechi hiyo.

Awamu ya pili iliwashuhudia Foxes wakikaribia kutingisha wavu katika dakika ya 60 kupitia kwa Jamie Vardy ambapo juhudi zake zilikwishia kwenye mlingoti.

Matokeo hayo yana maana kuwa wenyeji hao wa Old Trafford watajiunga pamoja na Chelsea, Man City na Liverpool katika kinyang'anyiro cha Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya kumaliza watatu kwenye jedwali.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved