Mlinda lango wa Man United Sergio Romero ataka kuruhusiwa kuondoka klabuni

Muhtasari

•Sergio Romero aomba wakuu wa Man United kuondoka katika klabu hicho

•Tayari ameanza kuppokea ombi kutoka kwa vilabu vingine huku wakiamini kazi na huduma zake

•Sergio aliwasaidia mashetani wekundu kubeba mataji matatu msimu uliopita

Sergio Romero
Image: Hisani

Mlinda lango wa Man United, Sergio Romero anaripotiwa kusihi klabu hiyo kumruhusu kuondoka, Romero amekuwa wa msaada mkubwa katika msimu uliopita wa klabu hicho hata baada ya kutosikizana na usimamizi wa klabu hicho.

Mzawa huyo wa Argentina alisaidia Mashetani Wekundu kubeba mataji matatu msimu uliopita ikiwemo ya Ligi ya Uropa na Kombe la FA.

Tayari nyota huyo mwenye miaka 33, amepigwa makasi kwenye kikosi cha United cha Ligi ya Mabingwa huku Henderson, Lee Grant na David de Gea wakipendelewa.

Kwa mujibu wa SunSport Kipa huyo amezungumza na wakuu wa klabu hicho cha Old Trafford ili kuzungumzia kuondoka kwake.

Inaaminika kuwa Romero yuko makini kutolipwa pesa zozote kabla ya kuhama licha ya United kuwa na deni lake la pauni 1.5 milioni.

Source: Getty Images Endapo klabu hiyo ya Manchester itakataa ombi lake, kipa huyo wa zamani wa Monaco atalazimika kusubiri hadi kukamilka kwa mkataba wake na United msimu ujao.

Hata hivyo, atakuwa na kibarua cha kuingia katika mkataba wa mkopo na klabu ya kigeni mapema mwezi Januari.

Tayari staa huyo ameanza kupokea ombi kutoka kwa vilabu kadhaa ambavyo vinatamani huduma zake.