Arsenal wapata kichapo kutoka kwa Burnley cha bao 1-0

Muhtasari
  • Bao la kujifunga la Pierre-Emerick Aubameyang katika awamu ya pili liliweka mwanya katika mechi ya Arsenal dhidi ya Burnley

Mechi kati ya Arsenal na Burnley ilisubiriwa sana na mashabiki huku wengi wakitabiri kwamba Arsenal wataibuka washindi katika mechi hiyo.

Bao la kujifunga la Pierre-Emerick Aubameyang katika awamu ya pili liliweka mwanya katika mechi ya Arsenal dhidi ya Burnley mnamo Jumapili, Disemba 1-0 huku mchezo huo ukitamatika 1-0.

Gunners walikuwa wanatarajia kutumia mechi hiyo kurejea katika mtindo wao wa ushindi baada ya kupokezwa kichapo cha 2-0 mechi yao ya awali dhidi ya Tottenham.

 

Hata hivyo, licha ya kutawala dakika za mapema za mechi hiyo, Arsenal walishindwa kupenyeza katika ngome ya Burnley ambao safu yao ulinzi ilibanwa vizuri.

Arsenal walikuwa na nafasi nzuri zaidi ya wazi kunako dakika ya 21 kupitia kwa Rob Holding ambaye alimalizia krosi iliyochanjwa na Saka akitumia kichwa.

Licha ya Arsenal kujikakamua na kuonekana wenye ujasiri mkubwa nguvu zao ziliambulia patupu baada ya yao kujifunga.

Mambo yaliwalemea Arsenal katika dakika ya 73 baada ya Aubameyang kuelekeza mpira kwenye lango lake kutokana na kona iliyochanjwa na Westwood.