'Familia yangu ilitishiwa mtandaoni,' - Mikel Arteta

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta
Image: Picha: BBC

 Meneja wa  Arsenal Mikel Arteta amedai kuwa familia yake ilitishiwa maisha mitandaoni, na ameiomba shirikisho la soka la Uingereza na serikali, kuongeza juhudi zao za usalama ili kuzuia madhara yeyote kwa familia za wachezaji, marefa na makocha.

Haya yanajiri siku moja tuu baada ya  shirkisho la soka na washika dau wa michezo kadhaa kuandikisha mkataba na wakurugenzi wakuu wa mitandao ya kijamii, ili kuwanasa wahalifu

Tukirudi nyumbani, mshambulizi wa AFC Leopards Elvis Rupia alitajwa kama mchezaji bora wa mwezi Disemba, katika ligi kuu ya FKF nchini.

 

Haya yanaijri baada ya kufunga magoli sita mwezi huo. Rupia ambaye sasa ana magoli 10 kutokana na mechi 9, alipata 50,000 na  amewashukuru wachezaji wenzake kwa kumwezesha kunyakua taji hilo.

Katika riadha, rais wa shirikisho la riadha nchini Jackson Tuwei, anasema AK wako tayari kwa kuandaa mbio za taifa za cross country katika uwanja wa Ngong Race Course leo asubuhi.  

Tuwei amewakumbusha wanariadha kutia bidii ili kufuzu kwa mbio za  Nyika za bara Afrika  zitakazo fanyika mwezi  Machi tarahe saba  7 mjini Lome, Togo.