Droo ya Europa: AC Milan kupambana na United, Arsenal yapewa Olympiakos

eufa europa
eufa europa

 Manchester United itapambana na  AC Milan katika awamu ya  16 bora ya ligi ya Uropa,   huku  Arsenali  ikikabana koo na  Olympiakos nao Tottenham wakimaliza udhia dhidi ya Dinamo Zagreb.

Kulingana na droo iliyotolewa jana, Rangers itapambana na  Slavia Prague,  Ajax ikialika Young Boys  nao  Dynamo Kiev wakipambana na Villarreal. Roma itapiga na Shakhtar Donetsk huku Granada ikialika  Molde.

Mkondo wa kwanza utachezwa Machi  tarehe 11 kabla ya mkondo wa pili kukamilika Machi 18.

Ufuatao ni msururu wa havari za spoti ulimwenguni.

Kwingineko, bwenyenye wa Chelsea Roman Abramovich amewapa wasmamizi wa klabu hio idhini  ya kuwania sahihi ya mshambulizi matata wa Norway  Erling Haaland msimu huu wa joto.

Nyota  huyo wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 20 amefanya vyema katika klabu hiyo tangu kujiunga nao kutoka  RB Salzburg mwezi Januari mwaka jana na inaaminika Abramovich yuko tayari kutoa zaidi ya pauni million 100 ili kumsajili.

Nahodha wa  Liverpool Jordan Henderson amefanyiwa upasuaji kutokana na jeraha alopata wakati walipoteza 2-0 dhidi ya Everton wikendi iliyopita ugani Anfield.  

Kiungo huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 30 sasa atasalia  nje kwa muda wa angalau mwezi mmoja na atarajea uwanjani mwezi Aprili. Kulingana na madaktari wa klabu hiyo Henderson atakosa mechi dhidi ya Sheffield United, Chelsea, Fulham na Wolves

Mbio za kwanza za msimu huu za  Track and Field  zitafanyika ugani Nyayo kesho asubuhi huku wanariadha kutoka kote nchini wakijumuika. Hapo awali mbio  hizo zilistahili  kufanyika katika chuo kikuu cha Bondo katika kaunti ya Siaya, lakini  AK iliamua kuzirejesha Nairobi kutokana na kanuni kali za covid-19 na ukosefu wa nafasi ya kutosha.