logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ligi ya Primia kuandikia vilabu kuwauliza maoni juu ya VAR

Ligi ya Primia inaandikia vilabu kuwauliza maoni makocha, wakurugenzi wa soka na manahodha juu ya VAR ikiwa na mtazamo wa kuborosha teknolojia hiyo msimu ujao. (Mail)

image
na Radio Jambo

Habari13 March 2021 - 08:40
images

Ligi ya Primia inaandikia vilabu kuwauliza maoni makocha, wakurugenzi wa soka na manahodha juu ya VAR ikiwa na mtazamo wa kuborosha teknolojia hiyo msimu ujao. (Mail)

Paris St-Germain wanafuatilia hali ya Cristiano Ronaldo huko Juventus na kuangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji huyo wa Ureno, 36, ikiwa ataamua kuondoka Turin. (Le Parisien - in French)

Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, atacheza misimu miwili zaidi barani Ulaya kabla ya kujiunga na Inter Miami ya MSL, huku uwezo wa mchezaji huyo kuendelea kusalia Barcelona hata baada ta msimu huu ukibashiriwa kuwa kwa asilimia 50 - 50. (Cadena Ser - in Spanish)

Chelsea inamnyatia winga wa Bayern Munich raia wa Ufaransa Kingsley Coman, 24, kama mwenye uwezekano wa kuchukua nafasi ya Christian Pulisic, wakati ambapo mchezaji huyo wa miaka, 22, raia wa Marekani ameonesha kuwa anataka kuondoka Stamford Bridge. (Mail)

Arsenal, West Ham, Everton na Brighton wanafanya mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Scotland,18, Ibane Bowat kutoka Fulham. (TeamTalk)

Ajenti wa Gianluigi Donnarumma, Mino Raiola inasemekana kwamba alianza mazungumzo na Chelsea na Manchester United kuhusu mlinda lango huyo wa AC Milan, 22. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia aliye San Siro utamalizika msimu huu. (Transfer Window Podcast, via Football London)

Kiungo wa kati Manchester United Nemanja Matic, 32, amesema atafikiria kurejea Benfica ikiwa kuna atakayemuhitaji, ingawa mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia anasisitiza kwamba ni mwenye furaha Old Trafford. (Sport TV, via Sun)

-Mkusanyiko wa habari kwa hisani ya BBC


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved