City yamtaka Joao Felix, Ronaldo huenda akarejea Santiago Bernabeu

ronaldo
ronaldo

Manchester City inafuatilia uhamisho wa mshambuliaji kinda wa Kireno wa klabu ya Atletico Madrid, 21, mshambuliaji Joao Felix kama mbadala wa Sergio Aguero, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Manchester City pia wanaongoza mbio za kumuwania mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway, 20 Erling Braut Haaland.

Lakini Barcelona wamemuweka Haaland kwenye orodha yake ya juu ya wacheza inaowawania katika dirisha lijalo la usajili, licha ya vilabu pia kuanza kujaribu kumsajili.

Baba wa Lionel Messi anatarajiwa kusafiri kwenda Barcelona jumatatu kukutana na rais wa klabu hiyo, Joan Laporta kujadili hatma ya mshambuliaji huyo muargentina, 33.

Manchester United itasikiliza ofa kwa ajili ya kipa wake raia wa Hispania David de Gea, 30.

Manchester United wako njia panda kuhusu kuongoza mkataba wa mshambuliaji wake raia wa Uruguay Edinson Cavani, huku maafisa tabibu klabuni hapo wakihuzunishwa na hali ya afya yake.

Wakala wa Cristiano Ronaldo, Jorge Mendes amezungumza na Real Madrid kuhusu uwezekano wa mshambuliaji huyo mreno huyo, kurejea Bernabeu kutokea Juventus.

Manchester United na Chelsea zinataka kumsajili mlinzi wa Roma na Italia, Gianluca Mancini, 24.

Mazungumzo kati ya mshambuliaji wa Brazil, Neymar, 29, na klabu yake ya Paris St-Germain kuhusu mkataba mpya wa miaka minne yanaendelea, huku pande zote mbili zikikitumai kufikiwa muafaka.

Tetesi hizi za soka ni kwa hisani ya BBC