Lionel Messi yuko tayari kusaini mkataba mpya Barcelona

messi
messi

Nyota wa Argentina Lionel Messi, 33,yuko tayari kusaini mkataba mpya Barcelona kufuatia uchaguzi wa rais mpya Joan Laporta, anadai nyota wa zamani wa Barcelona Rivaldo. (The Sun)

Arsenal hawana fursa ya kusaini mkataba wa kudumu na mchezaji wa Real Madrid anayecheza kwa mkataba wa mkopo Martin Odegaard, 22, huku klabu hiyo kubwa ya Uhispania ikiwa bado inamuangalia mshambuliaji huyo wa safu ya kati kama sehemu ya mipango yao ya muda mrefu . (Marca - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Liverpool Mholanzi Georginio Wijnaldum, 30, atahitaji kusubiri hadi Barcelona watakapomuachilia mchezaji wa kati Mbosnia Miralem Pjanic, 30, kabla hajakamilisha mkataba wake wa kuhamia Nou Camp. (Sport via Mirror)

Mshambuliaji wa Inter Milan na Ubelgiji Romelu Lukaku, 27, pia analengwa na meneja wa klabu ya Barcelona Ronald Koeman. (Calcio Mercato)

Liverpool wanaangalia uwezekano wa kumleta kikosini mchezaji wa safu ya mbele wa PSV Eindhoven Donyell Malen, licha ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 Mholanzi kusakwa na timu kubwa za Italia Juventus na AC Milan. (Gazzetta Dello Sport via Goal)

Meneja Ole Gunnar Solskjaer, 48, anatarajiwa kupata mkataba mpya hata kama Manchester United watamaliza msimu bila kushinda kombe . (Telegraph - subscription only)

Mmiliki wa klabu ya Sheffield United Prince Abdullah anasema hakutaka kumfukuza Chris Wilder na anadai meneja wa zamani wa Blades aliomba malipo ya pauni milioni 4 ajiuzulu. (Sky Sports

Egypt wametangaa kuwa wanamtaka Mohamed Salah kuunda sehemu ya kikosi chao cha mwisho kwa ajili ya michezo ya olympiki, hii ikimaanisha kuwa atakosa mechi za awali za maamndalizi ya msimu wa soka katika Liverpool. (Daily Mail)