Real Madrid yalaza Barcelona, Leeds yainyuka Man City

Benzema asherehekea kuifunga Barcelona katika mehi ya El Clasico picha: Hisani
Benzema asherehekea kuifunga Barcelona katika mehi ya El Clasico picha: Hisani

Licha ya kusalia wachezaji 10 uwanjani Real Madrid ililaza mahasidi wa Barcelona 2-1 na kupanda kileleni mwa La liga jana katika mechi ya kukata na shoka ya El Classico.

Karim Benzema aliweka Madrid kipao mbele katika dakika ya 13th kabla ya Toni Kroos kuongeza la pili dakika 15 baadae.

Mlinzi Oscar Mingueza alifungia Barca goli la kufuta machozi huku wakitafuta goli la kusawazisha kwa vyo vyote bila mafanikio.

Madrid ambao waliwakosa walinzi Sergio Ramos, Dani Carvajal na Rafael Varane walizuba makali ya Lionel Messi na wenzake, na kuongeza matumaini yao kutetea taji lao msimu huu.

Manchester City walishindwa kupanda alama 17 kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza baada ya kulazwa 2-1 ugani Etihad na Leeds United.

Stuart Dallas alifungia Leeds goli la ufunguzi katika kipindi cha kwanza kabla ya kuongeza la pili Kunako dakika la 91 baada  yaFerran Torres kusawazishia City katika kipindi cha pili.

Kwingineko, Chelsea ilinyorosha Crystal Palace 4-1 na kupanda hadi nafasi ya nne huku Christian Pulisic akifunga magoli mawili naye Kurt Zuma na Kai Havert wakiongoza goli moja kila mmoja naye  Benteke alifungia the Eagles goli la pekee.

Katika mechi nyengine ya 31 mabingwa Liverpool walitoka nyuma na kubwaga Aston Villa 2-1 na kulipiza kiasasi walipozabwa 7-2 katika mkondo wa kwanza. Alexander Arnold alifungia the reds goli la ushindi baada ya Mo Salah kusawazisha goli la  Ollie Watkins la ufunguzi.

Tukirejea nchini, wachezaji na maafisa wa kitengo cha ufundi katika timu 11 za ligi kuu nchini zenye makao yao mjini Nairobi walipata chanjo za Covid-19 ugani Kasarani jana huku wakitarajia ligi kurejea hivi karibuni baada ya kusitishwa na serikali.  

Mabingwa watetezi Gor Mahia, Tusker, AFC Leopards, Mathare United baadhi ya wengine sasa wanangoja chanjo ya pili inayotarajiwa baada ya angalau mwezi kupitia wizara wa afya, ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Timu tisa zenye makao yao katika makaunti tofauti zinatarajia chanjo hio kwanza leo.

Katika riadha, Emmanuel Naibei wa Kenya na Muithopia Mereset Dinke walinyakua mbio za Lagos City marathon jana nchini Nigeria.

Naibei alitimuka kwa masaa mawili na dakika 11 na kushinda dollar za Merikani 30,000. Deresa Galala alimaliza wa pili huku mwenzake wa Ethiopia alimaliza wa tatu.

Upande wa wanawawake, Dinke alifuatwa kwa karibu na Mkenya Celestine Chep Chir Chir na Desa Mulune katika nafasi ya pili na tatu mtawalia.