Kapu la soka: Gor yasusia mazoezi wakidai mishahara ya miezi mitatu

divas
divas

Wachezaji wa Gor Mahia wamsusia mazoezi huku wakidai mishahara yao ya miezi tatu. Licha ya kuwa serikali imepiga marufuku michezo kote nchini ili kuzuia kuenea kwa virusi vya korona, KO'gallo walikua wanafanya mazoezi mitandaoni kupitia zoom. Hata hivo vijana hao waliamua kususia mazoezi hadi walipwe pesa zao.

Kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel anasema vijana wake wanajiamini kufanya vyema dhidi ya Real Madrid, baada ya kuwanyuka West Ham ba 1-0 na kuweka nafasi yao thabiti katika nne bora.

Bao la kwanza la Timo Werner tangu mwezi Februari liliwapa the Blues ushindi na kuwabandua the Hammers, kumaanisha kua the Blues watasafiri hadi Uhispania wakiwa na matumaini makubwa kwa mechi ya nusu fainali ya Jumanne ya ligi ya mabingwa dhidi ya Madrid ambao ni washindi mara 13.

Joe Willock alisawazisha katika dakika ya 95 na kusaidia Newcastle  kujizolea sare ya 1-1 dhidi ya Liverpool. Mo Salah aliwapa Liverpool uongozi kabla ya Willock kusawazisha, na kudunisha nafasi yao ya kumaliza katika nafasi ya nne bora. 

Arsenal wanaaminika kumtaka kiungo wa Borussia Dortmund Julian Brandt, iwapo watakosa kumsajili Martin Odegaard kutoka Real Madrid. Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 24, amekua akiwindwa na the  Gunners kuanzia Januari lakini Dortmund walikataa kumuuza na hivyo kumleta Odegaard kwa mkopo.  

Leeds  wataalika Manchester United katika mechi ya kukata na shoka ya EPL ugani  Eland road mwendo wa 4pm. United ambao wana wania kupunguza idadi ya alama ya viongozi Man City kileleni hadi alama tisa watazikosa huduma za  Marcus Rashford, huku Leeds ambao wameshinda mechi tano kwa mpigo, wakicheza bila Raphinha na Rodrigo.

Sergio Aguero huenda akacheza finali yake ya mwisho ugani Wembley wakati  Manchester City, itakabana koo na  Tottenham katika fainali ya  carabao cup ugani Wembley.  Mzaliwa huyo wa Argentina  amekua nje kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na majeraha, la msuli. 

Kiungo Kevin De Bruyne pia anatarajiwa kurejea baada ya kujeruhiwa katika ushindi wao dhidi ya  Aston Villa.