Mlinzi Joseph Okumu anamezewa mate na Napoli, Rangers na Valencia

Joseph Okumu picha: The-star
Joseph Okumu picha: The-star

 Mlinzi wa  Harambee stars Joseph  Okumu amehusishwa na vilabu kadha za bara  ulaya huku mabingwa wa Scotland Rangers wakiwa kipao mbele.  

Okumu ambaye anachezea Elfsborg ya daraja la kwanza la Uswizi Pia anamezewa mate na  Napoli, Valencia na  Nice huku wakala wake wakiendelea na mazungumzo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye hapo awali alichezea  Chemilil sugar amekua katika hali dhabiti msimu huu akichezea Kenya na klabu yake.

Mshambulizi wa  Brazil Wilson Silva amegura klabu ya  Gor Mahia miezi minne tuu baada ya kuandikisha mkataba wake wa mwaka mmoja.

Silva aliondoka wiki iliyopita na kurejea kwao Rio kutokana na  kutolipwa mishahara ya miezi kadha na senti za kuandikisha sahihi. Silva mwenye umri wa miaka 20 alifunga magoli mawili kutokana na mechi tano.

Chelsea na Manchester City wanawania sahihi ya  mshambulizi wa  Bayern Munich Robert Lewandowski.

Miamba hao wawili wa Uingereza watapambana katika fainali za klabu bingwa bara ulaya tarehe 29 mwezi huu na wanatarajiwa kutoa pauni millioni 60 ili kupata huduma zake.  

Mzaliwa huyo wa Poland mwenye umri wa miaka  32  amefunga magoli 272 akichezea  Borussia na Dortmund Bayern mtawalia katika Bundesliga.

FIFA, kwa kushirikiana na CAF, imeahirisha mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA Qatar 2022 ambazo zilikuwa zimepangwa Juni.

Mechi za kufuzu sasa zimepangwa kufanyika mnamo Septemba, Oktoba na Novemba 2021, na Machi 2022. FIFA inasema hii ni kutokana na janga la COVID-19, na hitaji la kuhakikisha hali nzuri ya kucheza kwa timu zote.