logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mamake Ronaldo angependa nyota huyo kurejea Sporting Lisbon

Mama mzazi wa Cristiano Ronaldo, Dolores Aveiro, angependa mtoto wake huyo anarejea katika klabu ya Sporting Lisbon, ya Ureno iwapo mchezaji huyo ataondoka katika kabu ya Juventus majira ya joto. (Guardian)

image
na Radio Jambo

Burudani14 May 2021 - 06:47
Cristiano Ronaldo na mamake mzazi

Mama mzazi wa Cristiano Ronaldo, Dolores Aveiro, angependa mtoto wake huyo anarejea katika klabu ya Sporting Lisbon, ya Ureno iwapo mchezaji huyo ataondoka katika kabu ya Juventus majira ya joto. (Guardian)

Kiungo wa zamani wa Barcelona Xavi amesaini mkataba mpya ya kuendelea kuifundisha klabu ya Al-Sadd ya Qatar hadi 2023, Kuongeza mkataba kwa Xavi ni pigo kwa rais wa Barca Joan Laporta, ambaye anatafuta kocha wa kuchukua nafasi ya bosi wa sasa Ronald Koeman. (Il Milanista - in Italian)

Mlinzi wa Kati RB Leipzig's Dayot Upamecano, 22, ambae atajiunga na mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich baada ya ligi kumalizika, amesema alikata nafasi ya kusajiliwa na Manchester United alipokuwa na miaka 17. (The Athletic - subscription needed)

Manchester United inaanda dau la pauni million 68 kwa ajili ya kiungo Marcos Llorente, wa Atletico Madrid's, huku Atletico wenyewe wakitaka kuharakisha mchakato wa kumsainisha mkataba mpya kiungo huyo ili aendelee kusalia katika klabu hiyo (Mirror)

Leicester City wanavutiwa na kumsajili mlinzi wa kushoto wa Southampton Muingereza Ryan Bertrand ambaye mkataba wake unakwisha mwishoni mwa msimu huu baada ya kuwatumikia Southapton kwa miaka saba (Leicester Mercury)

Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone anatajwa kuwa mshabiki mkubwa wa kiungo wa Liverpool Naby Keita, 26, na anapenda kumuongeza mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea katika kikosi chake (Fichajes via Star)


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved