Mason Mount ndiye mchezaji bora Chelsea msimu huu

Mount amepewa tuzo la mchezaji bora kwenye timu ya wanaume baada ya kuisaidia timu kufika fainali mbili.

Muhtasari

Mount amepewa tuzo la mchezaji bora kwenye timu ya wanaume baada ya kuisaidia timu kufika fainali mbili.

Mason Mount
Mason Mount
Image: Hisani

Kiungo mshambulizi wa timu ya Chelsea, Mason Mount ameshinda tunzo la mchezaji  bora katika klabu hiyo msimu huu.

Mchezaji huyo raia wa uingereza na ambaye  ana miaka 22 amelishinda tuzo hilo baada ya kusaidia klabu hiyo kufika fainali mbili ikiwemo ya kombe la FA na kombe la mabingwa Ulaya(Champions League)

Mount ameifungia klabu ya Chelsea mabao sita na kusaidia kufungwa kwa mabao tano katika kombe la EPL huku akiwa mfungaji bora wa pili katika klabu hiyo.

Huku akipokea tuzo hilo, Mount amekisifia chuo cha kufunzia kandanda cha Chelsea na kushukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kumuunga mkono.

"Niwekea wakfu tuzo hili chuo cha kufunzia kandanda cha Chelsea na nawashukuru mashabiki wa timu hii kwa upendo mnaoendelea kunipa" Mount alisema.

Kwa sasa Chelsea imeshikilia nambari tatu ikiwa na alama 67 ikiwa nyuma ya Manchester United na Manchester City.