FKFPL: Tusker yapoteza nafasi ya kupanda alama 6 kileleni mwa ligi

Tusker fc Timothy Otieno. Picha: The Star
Tusker fc Timothy Otieno. Picha: The Star

Tusker walikosa kupanda alama sita kileleni mwa ligi baada ya kutoka sare ya 1-1 na KCB  katika mechi ya ligi ya FKF jana.  Sammy Mejaa aliweka Tusker  mbele kunako dakika ya nne kabla ya Kevin Kimani kusawazishia Wazito katika dakika ya 21.

Wana mvinyo hao sasa wako alama nne mbele ya  KCB baada ya mechi 18.

Kiungo wa Kenya  Henry Ochieng ameondoka klabu ya Watford, baada ya kujiunga nao mwezi Januari, kutoka Cork City ya Ireland kwa mkopo.

Ochieng  ni mmoja kati ya wachezaji 13 waliotemwa kwani hawakua katika mipango ya Watford baada ya kupandishwa kurejea  EPL msimu huu.  Ochieng mwenye umri wa miaka 22  alichezea Harambee stars ya vijana wasio zidi umri wa miaka 23 dhidi ya Mauritius.

Mwenyekiti wa shirikisho la michezo ya shule za upili nchini Peter Orero amewahakikishia wanafunzi na walimu kuwa michezo ya shule itarejea mwaka huu, baada ya kusitishwa tangu  mwaka jana kufuatia mchipuko wa janga  la corona. 

Hii ni kufuatia mikutano kati ya maafisa wa michezo nchini na wizara ya elimu mjini Nakuru. Orero amesema watahakikisha wanafuata kanuni  za covid-19 ipasavyo  ili kuzuia maambukizi zaidi.

Kocha  wa kikosi cha wanawake nchini cha voli boli Paul Bitok  ana wasiwasi kutokana na ukosefu wa mechi za kirafiki  na mazoezi ya  nje kama ilvyoratibiwa hapo awali.  

Malkia Strikers  walifaa kuelekea Brazil kwa mazoezi na  mechi kadhaa za kirafiki lakini safari ilitibuka kutokana na  mchipuko wa janga la korona. Timu hiyo imo kambini katika uwanja wa Kasarani.