FKFPL: Homeboyz yanyuka W Stima, Leopards watoka sare na Rangers

afc leopards vs posta rangers
afc leopards vs posta rangers
Image: hisani

AFC Leopards  ilikosa nafasi ya kupunguza idadi ya alama za Tusker kileleni hadi tatu baada ya kutoka sare tasa na Posta Rangers katika mechi ya ligi kuu ya FKF.

Kwingineko  Masita Masuta na Clinton Omondi walifunga goli moja kila mmoja na kusaidia Ulinzi stars kuinyuka  Kariobangi Sharks 2-0 huku Kakamega Homeboyz ikinyuka Wester stima mabao  4-0.

Zifuatazo ni za tetesi za soka Ulaya kwa hisani ya BBC.

Mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 32, amekubali mkataba wa miaka miwili kujiunga na Barcelona wakati mkataba wake wa Manchester City utakapomalizika mwishoni mwa msimu. (Guardian)

 

sergio 1
sergio 1

Mchezaji wa Tottenham aliye katika uhamisho wa mkopo Gareth Bale, 31, anafikiria kustaafu mkataba wake wa Real Madrid utakapomalizika mwishoni mwa msimu ujao(AS)

Tottenham watajaribu kumshawishi bosi wa Leicester, Brendan Rodgers, 48, kuwa meneja wao mpya ikiwa wolves watashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa (Sun)

Leicester wanaongoza harakati za kumsajili mshambuliaji wa Celtic Odsonne Edouard, ingawa Arsenal, Newcastle na Aston Villa pia wanamtaka Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 23. (Daily Record)

West Ham wanataka kusalia na mshambuliai anayewachezea kwa mkopo wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28. (Mail)

cvqsttnwiaaycto
cvqsttnwiaaycto

Kocha ajaye wa Roma, Jose Mourinho ameionya Manchester United kwamba hatalipa kiasi cha juu cha fedha kuliko thamani yake kiungo wa Serbia mwenye umri wa miaka 32 Nemanja Matic. (Corriere dello Sport via Mirror)