Sancho ataigharimu Man United pauni milioni 81.5

sancho. bbc
sancho. bbc

Tetesi za soka bara Uropa;

Manchester United wameambiwa kuwa itawagharimu kiasi cha pauni milioni 81.5 kumsajili winga Jadon Sancho,21, kutoka Borussia Dortmund. (Mirror)

Tottenham itafanya mazungumzo zaidi na kocha wa Ajax Erik Ten Hag,51, baada ya kushindwa kufanikisha uhamisho wa Antonio Conte. (Mirror)

Duncan Ferguson, 49, amekataa kazi ya ukufunzi Real Madrid kwasababu atanaka kuwa kocha wa Everton. (Sun)

West Ham wanaamini kuwa David Moyes atasaini mkataba mpya wa kudumu baada ya kufanya mazungumzo na kocha huyo ambaye amehusishwa na tetesi za kurejea Everton. (Football Insider)

Mlinzi wa kulia wa Atletico Madrid Kieran Trippier,30, amewaambia wachezaji wenzake wa England yuko na mpango wa kujiunga na Manchester United msimu huu. (Mirror)Barcelona wanafikiria kutoa ofa iliyoboreshwa kwa kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum,30, ambaye anajiandaa kuondoka Liverpool kwa uhamisho huru, baada ya Paris St-Germain kupoteza ofa ya awali ya Barca.(Marca - in Spanish)

Ikiwa Barcelona haitakamilisha usajili wa Wijnaldum na Memphis Depay, 27, wa Uholanzi kutoka Lyon wiki ijayo inaweza kuwauza hadi wachezaji wanne. (Sport - in Spanish)

Kocha mpya wa Roma Jose Mourinho anataka kumsajili mmoja kati ya walinda mlango watatu: Hugo Loloris,34, wa Tottenham, Wojciech Szczesny, 31, wa Juventus au Rui Patricio wa Wolves,33. (La Gazetta dello Sport-in Italian)Mchezaji wa Arsenal Granit Xhaka, 28, anasalia kuwa mtu anayelengwa zaidi na Roma katika eneo la kiungo wa kati. (Corriere dello Sport-in Italian)

Kwa hisani ya BBC