(+Video)Gari la mmoja wa madereva wa WRC Safari Rally labingiria

Muhtasari
  • Gari la mmoja wa madereva wa WRC Safari Rally labingiria
Image: Twitter

Tejveer Rai, bingwa wa WRC Safari Rally alishindwa kukamilisha mbio yake Ijumaa asubuhi baada ya gari lake lilikokuwa linaenda kwa  kasi kuanguka.

Bingwa wa rally alikuwa akiendesha gari la Volks GTI polo wakati uande mmoja wa gari lake ulichimba chini, na kusababisha gari kubigiria mara tatu.

Tejveer, ambaye ni wa Kenya alikuwa katika gari na dereva wake Gareth Dawe.

Watazamaji na mameneja wa tukio walikimbilia mahali pa ajali hiyo na kuwaokoa.

Hakuna majeruhi yaliyoripotiwa wakati huo.

Michuano ya Ijumaa inahusisha sehemu ya madereva 2 na 3, na inafanyika kwenye Hifadhi ya Huduma katika Naivasha (Chui Lodge 1 na 2, Kedong 1 na 2 na Oserian 1 na 2)

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Nairobi Esther Passaris  kupitia kwenye twitter alisema kwamba anafuraha kusikia kwamba Tejveer na dereva wake wako salama.

Hii hapa video ya tukio hilo;