Raundi ya 16 ya michuano ya kuwania kombe la Carabao ilichezwa siku ya Jumanne na Jumatano wiki hii.
Michuano hiyo imeingia katika raundi ya nne huku Arsenal, Chelsea, Manchester City, Tottenham, Liverpool, Westham, Leicester, Brighton, Burnley, Leeds, Preston, Southampton, Stoke City, Brentford, QPR na Sunderland zote zikifuzu.
Mashetani wekundu walibanduliwa nje ya uwaniaji kombe hilo usiku wa Jumatano baada kuchapwa 0-1 nyumbani na West Ham. Bao la pekee lilifungwa na Manuel Lanzini katika dakika ya tisa.
Chelsea walilaza Aston Villa mabao mawili kwa moja na kufuzu kuingia raundi ya 4 huku majirani Arsenal wakipata ushindi wa 3-0 dhidi ya AFC Wimbledon.
Manchester City walipata ushindi mkubwa wa 6-1 dhidi ya Wycombe, Southampton wakachapa Sheffield 3-2, Fulham wakapoteza 0-1 dhidi ya Leeds, Tottenham wakashinda Wolves 3-2, Leicester wakapiga Milwall 2-0 ugenini.
Brighton walihitimu baada ya kushinda Swansea 2-0, Burnley wakalaza Rochdale mabao 4 kwa 1, Preston wakapiga Cheltenham 4-1, Watford wakapoteza 1-3 dhidi ya Stoke City na Sunderland ikapiga Wigan 2-0.
Raundi ya nne ya michuano hiyo itachezwa mwishoni mwa mwezi Oktoba.