logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pogba apata jeraha baya la nyonga

Pogba hatoshiriki katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Kazakhstan ama mechi ya ugenini

image

Michezo09 November 2021 - 14:00

Muhtasari


  • Pogba hatoshiriki katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Kazakhstan ama mechi ya ugenini dhidi ya Finland Novemba 16

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba hatoshiriki katika mechi ya michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia baada ya kupata jeraha la nyonga.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia , mwenye umri wa miaka 28alipata jeraha wakati wa mazoezi siku ya Jumatatu , Shirikisho la soka nchini Ufaransa FFF limesema.

Pogba hatoshiriki katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Kazakhstan ama mechi ya ugenini dhidi ya Finland Novemba 16.

Tayari alitarajiwa kukosa mechi ya United ugenini dhidi ya Watford katika ligi ya Premia tarehe 20 Novemba , huku akikamilisha marafuku yake ya mechi tatu .

Pogba alipokea marufuku hiyo kabla ya kutolewa nje wakati wamechi ya kichapo cha 5-0 dhidi ya Liverpool tarehe 24 mwezi Oktoba.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved