Kwa nini makocha wa ligi kuu England wanatimuliwa?

Muhtasari
  • Kwa nini makocha wa ligi kuu England wanatimuliwa?
  • Kubadilisha makocha katikati ya msimu kama sasa ni biashara ya hatari
Image: BBC

Ligi kuu ya England kama ilivyo kwa ligi nyingine kubwa, iko mapumzikoni kwa siku kama 12 kupisha michezo ya kimataifa kwa ya kufuzu kombe la dunia.

Mpaka inasimama mwishoni mwa juma, mechi 11 za ligi zilikuwa zimeshachezwa kwa msimu huu huku tayari mameneja watano wakifungashiwa virago, watatu wakifukuzwa ndani ya juma moja.

Kutimuliwa kwa makocha England nini kinaendelea?

Kufukuzwa kwa Dean Smith, aliyekuwa anainoa Aston Villa kunamaanisha kuwa mameneja wengi wamepoteza kazi katika ligi kuu ya England msimu huu kuliko msimu mzima wa 2020-21 - hii ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya kufukuzwa kwa makocha katika hatua hii ya kampeni (mechi 11) katika kipindi cha miaka 17.

Kila mtu anatoa sababu zake, wengine wakisema pengine ni kwa sababu ya kurudi kwa hamasa ya mashabiki baada ya janga la korona, hofu pamoja na shinikizo la kifedha.

Kutimuliwa kwa idadi hii ya makocha si kawaida, Je tumefikaje hapa?

Robo ya vilabu vyote vya Premier League vimebadilisha kocha wao hadi kufikia sasa msimu huu, huku watatu wakifukuzwa kazi kwa haraka katika kipidi cha hivi karibuni.

Oktoba 3, 2021: Xisco Munoz wa Watford alikuwa wa kwanza kutimuliwa, alifukuzwa wakati timu hiyo ikiwa katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi, timu hiyo ikiwa imecheza mechi saba tu. Nafasi yake ilichukuliwa na Claudio Ranieri.

Oktoba 20, 2021: Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce alikubaliana na klabu hiyo kuachia ngazi, ikiwa ni siku 13 baada ya matajiri wapya wa Saudi Arabia kuinunua timu, huku klabu hiyo ikiwa haijashinda mchezo hata mmoja kwenye ligi. Nafasi yake imechukuliwa na Eddie Howe.

Novemba 1, 2021: Tottenham ilimfukuza Nuno Espirito Santo baada ya miezi minne kwenye wadhifa huo, baada ya matokeo yasiyoridhisha ya kufungwa mechi tano katika mechi saba za ligi wakati huo. Nafasi yake ilichukuliwa na Antonio Conte.

Novemba 6,2021: Daniel Farke wa Norwich alitimuliwa saa chache baada ya ushindi wao wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu. Klabu bado haijamteua mrithi wake mpaka sasa.

Novemba 1: Kocha wa Aston Villa Dean Smith alifukuzwa kazi siku mbili baada ya klabu hiyo kushindwa katika michezo mitano mfululizo kwenye ligi. Bado haijatangazwa mbadala.

Katika misimu mitatu iliyopita, kila msimu ni timu moja tu ndiyo ilikuwa imeachana na kocha wake kufikia hatua kama hii ya mechi 1.

Msimu wa Ligi kuu ambao ulishuhudia makocha wengi wakitimuliwa Ligi Kuu ni ule wa 2013-14 na 2017-18, ambapo walitimuliwa makocha 10 kwa kila msimu.

Je kutimua makocha ni muarobaini?

Kubadilisha makocha katikati ya msimu kama sasa ni biashara ya hatari.

Hata hivyo, hilo halivizuii vilabu kufukuza ama kuachana na makocha wake - kumekuwa na mabadiliko 16 ya makocha tangu kuanza kwa kampeni ya 2019-20.

Kimsingi kubadilisha makocha wakati wa msimu ukiendelea huleta matokeo mchanganyiko. Kwa upande wa msimamo wa ligi, Tottenham walinufaika zaidi walipomtoa Mauricio Pochettino na kuchukua nafasi ya Jose Mourinho, ambaye alisimamia kupanda kwa nafasi nane kutoka nafasi ya 14 mpaka nafasi ya 6 katika msimu wa 2019-2020

Baadaye msimu huo, uamuzi wa Everton wa kumfukuza Marco Silva huku klabu hiyo ikiwa kwneye hatari ya kushuka daraja kabla ya bosi wa muda Duncan Ferguson kuthibitishwa kushika mikoba na kuisadia klabu hiyo hadi nafasi ya 15 kabla ya Carlo Ancelotti kuipaisha hadi ya 12.

Msimu wa 2018-2019 Arsenal limtimua Unai Emery na kumleta nahodha wake zamani aliyeko mpaka sasa, Mikael Arteta, hata hivyo kimsimamo Emery alimaliza msimu Arsenal ikishika nafasi ya 8, ilimaliza pia katika nafasi hiyo hiyo katika msimu uliofuata wa 2020-2021 chini ya kocha mpya Arteta.

Kuwasili kwa Thomas Tuchel kama mbadala wa Frank Lampard katika klabu ya Chelsea mwezi Januari pia kuliiboresha timu hiyo, huku Mjerumani huyo akifanikiwa kuipaisha Chelsea mpaka nne bora kabla ya kuwaongoza The Blues kutwaa taji lao la pili la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini Watford iliwatimua makocha watatu - Javi Gracia, Quique Sanchez Flores na Nigel Pearson - katika msimu wa 2019-2020. Pearson alipofukuzwa, Hornets walikuwa na alama tatu juu ya mstari kushuka daraja zikisalia mechi mbili, na kocha wa muda Hayden Mullins alishindwa kuinusuru klabu hiyo.

Ligi kuu ya England kama ilivyo kwa ligi nyingine kubwa, iko mapumzikoni kwa siku kama 12 kupisha michezo ya kimataifa kwa ya kufuzu kombe la dunia.

Mpaka inasimama mwishoni mwa juma, mechi 11 za ligi zilikuwa zimeshachezwa kwa msimu huu huku tayari mameneja watano wakifungashiwa virago, watatu wakifukuzwa ndani ya juma moja.

Wali hapa nini kinaendelea?

Kufukuzwa kwa Dean Smith, aliyekuwa anainoa Aston Villa kunamaanisha kuwa mameneja wengi wamepoteza kazi katika ligi kuu ya England msimu huu kuliko msimu mzima wa 2020-21 - hii ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya kufukuzwa kwa makocha katika hatua hii ya kampeni (mechi 11) katika kipindi cha miaka 17.

Kila mtu anatoa sababu zake, wengine wakisema pengine ni kwa sababu ya kurudi kwa hamasa ya mashabiki baada ya janga la korona, hofu pamoja na shinikizo la kifedha.

Shinikizo la kifedha na mashabiki

Ukisalia katika ligi ya England kuu na kudumu ni jambo muhimu kifedha , kwa sababu timu ikishuka kunakuwa na upotevu mkubwa wa mapato ya TV- mkataba wa sasa wa TV ni £4.7bn.

Hilo moja, jambo la pili i athari za Janga la korona, ambalo limevigharimu vilabu 20 tajiri zaidi barani Ulaya zaidi ya pauni bilioni 1.7 kufikia mwisho wa msimu uliopita, kwa mujibu wa kampuni ya fedha ya Deloitte.

"Tunashuhudia upande wa pili wa biashara kubwa ya soka kwa sasa," anasema kiungo wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza Nigel Reo-Coker.

"Vilabu vingi vinataka suluhu hiyo ya haraka. Nadhani ni zaidi kuhusu faida ya kifedha sasa kuliko kitu kingine chochote."

Je, kurudi kwa mashabiki kwenye viwanja pia kumechangia presha ya kufukuzwa kwa makocha?

Mwaka jana, Arsenal walicheza mechi saba bila kupata ushindi wowote kwenye ligi, na mechi nyingi walicheza bila mashabiki, na kocha wake Mikel Arteta alisalia klabuni hapo.

Nuno hakuwa na bahati hiyo. Mreno huyo, ambaye alikuwa amepewa mikoba mwezi Agosti, alifukuzwa kazi baada ya kupoteza michezo mitatu kati ya minne, na timu yake kuzomewa na mashabiki katika mchezo wake wa mwisho akiwa kocha.

Makocha gani wengine wamekalia kuti kavu?

Iko wazi kwa namna mambo yalivyo makocha kama Ole Gunnar Solksjaer wa Manchester United, Sean Dyche wa Burnley na Thomas Frank wa Brentford wako mguu ndani mguu nje kwenye vilabu vyao.

Solksjaer anashinikizo kubwa zaidi kwa sababu amepewa fedha za usajili na kusajili kila aliyemtaka wakiwemo Jadon Sancho, Cristiano Ronaldo na Raphael Varane lakini matokeo ya hivi karibuni hayaakisi ukubwa wa timu hiyo na uwezo wa majina wa wachezaji wake.

Sean Dyche ndiye meneja aliyekaa muda mrefu zaidi kwenye Premier League, akiwa ameinoa Burnley tangu Oktoba 2012, lakini hilo alimuondoi kwneye hatari ya kutimuliwa kwa sababu timu hiyo imekusanya alama 8 tu baada ya kushinda mchezo mmoja na kutoka sare mitano, ikiwa miongoni mwa wimu 3 zilizo kwenye hastari ya kushuka daraja

"Dunia inabadilika - hakuna msimamo wa kati tena," alisema bosi huyo wa zamani wa Stoke na West Brom.

"Mashabiki wanaotaka kuona makocha wakibadilishwa ndio wanaoleta kelele." Aliongeza

Mikel Arteta alikuwa miongoni mwa makocha waliokalia kuti kavu mezi uliopita lakini kutofungwa katika michezo 10 mfululizo kwenye mashidano yote, akizifunga pia Spurs na Leicester kumemshusha pumzi kiasi, ingawa mechi ujao dhidi ya Liverpool utakuwa mtihani muhimu wa kupima uwezo wake kwenye soka la kiwango cha juu.