logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Simbas wafanya mazoezi kabla ya kukabiliana na Namibia kwenye mechi ya Marudio

''Tunapanga  kuanza mazoezi mwezi ujao na  kukagua baadhi ya maeneo ambayo yalituangusha katika mechi dhidi ya Namibia,''

image
na Davis Ojiambo

Michezo20 July 2022 - 05:03

Muhtasari


  • •Simbas ilishindwa kujinyakulia tiketi ya moja kwa moja ya kufuzu kwa Afrika,
Mchezaji wa Simba wa Kenya Isaac Njoroge akicheza dhidi ya Uganda katika mechi iliyopita ya Kombe la Elgon

Baada ya kukosa kufuzu kwa Kombe la Dunia la Raga, Kenya Simbas sasa wameanza zoezi yao kwa mnajili ya marudio yatakayofanyika Novemba huko Dubai.

Simbas ilishindwa kujinyakulia tiketi ya moja kwa moja ya kufuzu kwa Afrika, kwa kufungwa na Namibia mabao 36-0 kwenye fainali iliyochezwa Marseille, Ufaransa.

Kocha mkuu wa Simbas Paul Odera alisema timu hiyo inapanga kuwa na kambi nne za mazoezi kabla ya marudio. Odera alisema anaamini kuwa kambi hizo zitakuwa muhimu kwa Kenya katika mchujo wa mwisho.

“Tunapanga  kuanza mazoezi mwezi ujao na  kukagua baadhi ya maeneo ambayo yalituangusha katika mechi dhidi ya Namibia,” alisema Odera.

Alisema wana nia kubwa ya kuboresha safu, kukaba moja kwa moja na ufanisi katika ushambuliaji.

"Wavulana walifanya vyema katika dakika ya 20 lakini hatukuweza kufanya mashambulizi dhidi ya  Namibia kwa hivyo walitumia nafasi hiyo kutushambulia zaidi," alibainisha.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 alisema watalazimika pia kuboresha upigaji teke ambao haikuzingatiwa  kwenye fainali.

Simbas ambao wako nafasi ya 33 watakabiliwa na upinzani wa hali ya juu nchini Marekani ambao wako nafasi ya 19, Ureno (20) na ama Tonga (18) au Hong Kong (21) katika marudio.

Odera alisema hawana cha kuogopa. "Ikiwa tutafanya maandalizi thabiti na kucheza mechi kadhaa za maandalizi basi sina shaka tutafanya vyema," aliongeza.

Kocha huyo aliridhishwa na kiwango cha kazi na uchezaji wa washambuliaji haswa wakati wa mchujo.

Odera ana matumaini kuwa timu hiyo itapata mechi za kirafiki kabla ya marudio.

"Ni muhimu tucheze mechi kadhaa za maandalizi kabla ya kurudiwa ili kujaribu mifumo yetu na kushughulikia udhaifu wetu."

Simbas walicheza katika marudio ya Kombe la Dunia 2019, wakipoteza mechi zote nne kwa Ujerumani 43-6, Canada 65-19 na Hong Kong 42-17.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved